KWARESMA YAANZA RASMI JANA
Na:Alfred Lukonge Waumini wa dini ya kikristo duniani kote siku jumatano wataadhimisha siku ya majivu kama ishara ya kuanza kwa kipindi cha Kwaresma ambacho huambatana na kufunga kama ishara ya kukumbuka mateso ya mwokozi wao Yesu kristo. Akizungumza na SAYUNIMEDIA Mch. Kiongozi kutoka KKKT usharika wa Kigogo jijini Dar es Salaam Richard Hananja amesema lengo la kipindi hiki cha kanisa ni watu wapate kutubu kwa kuwa wayahudi wa enzi hizo walitumia majivu kama ishara ya toba wapate kupewa msamaha wa dhambi. MCHUNGAJI RICHARD HANANJA.