Na:Alfred Lukonge Ikiwa imebaki miezi mitatu na wiki mbili kabla ya Kwaya ya Uinjilisti ya Sayuni kutoka KKKT usharika wa Majengo kufanya uzinduzi wa albamu yao mpya ya sauti iliyobatizwa jina la Beberu tukio linarotarajiwa kufanyika tarehe 10/6/2018, SAYUNIMEDIA ilifunga safari kwenda kuongea na mwalimu mwandamizi wa kwaya hiyo Bi.Elinju Makalla kujua namna gani wanakwaya wake wamejiandaa kuelekea uzinduzi huo pamoja na mambo mengine ya kiroho. Akizungumzia uzinduzi huo Bi.Makalla amebainisha kuwa kuelekea siku hiyo mambo yanaenda vizuri kwa wanakwaya kupokea mafundisho wanayopewa kwa weledi wa hali ya juu na kutoa wito wa watu kujitokeza kwa wingi ili waone kwaya ya Sayuni imekuja na kitu gani kipya. Mwalimu Mwandamizi wa Kwaya ya Uinjilisti ya Sayuni kutoka KKKT Usharika wa Majengo Elinju Makalla akiwa katika pozi alipotembelewa na mwandishi wa habari hii nyumbani kwake