MAJENGO YAADHIMISHA PENTEKOSTE
Na:Alfred Lukonge
Hapo
jana Jumapili ya tarehe 21/5/2018 ilikuwa ni siku ya kusheherekea Pentekoste
ambapo kwa mujibu wa imani yetu ya kikristo, tunakumbuka jinsi Roho Mtakatifu
alivyoanza kufanya kazi rasmi hapa Duniani kama Bwana wetu YESU Kristo alivyohaidi
kuwa akiondoka atatuachia msaidizi tukiongozwa na mistari ya Biblia kutoka (MDO 2:17-21)
Akitoa
neno la mahubiri kwenye kanisa la KKKT Usharika wa Majengo lililopo Kihonda
Dayosisi ya Morogoro Parish Worker wa usharika huo Bi.Happy Merry amebainisha
kuwa watu wa kanisa wanatumia kigezo cha Roho Mtakatifu kwa kunena kwa lugha
ndivyo sivyo, kwani Roho Mtakatifu akimtokea mtu lazima kuwe na mtafsiri kwa
minajili ya watu waliopo karibu kuelewa kile kitu ambacho anakinena.
Bi.Happy Merry akitoa neo la mahubiri katika ibada hiyo.
Parish.Merry
pia amebainisha kuwa siku za hivi karibuni watu wanaanzisha makanisa
na kuwaaminisha watu kuwa wana Roho
Mtakatifu kumbe roho mtaka vitu na kujinasibu kuwa watu wakienda kwao awatatoka
kama walivyokuja jambo ambalo wakati mwingine
sio kweli na kuishia kuwaibia watu.
Amesema
kuwa kwa mkristo thabiti Roho Mtakatifu umeondolea hofu kwa kitu chochote
atakachonuia kukifanya ikiwemo
kumuongoza kuomba maombi yenye mashiko pamoja na kumsimamisha kwenye njia za
Mungu wa kweli tofauti na miungu mingine.
Katika
ibada hiyo kulikuwa na tukio la kuwakumbusha washarika na watu mbalimbali waliochukua kadi
ili kuchangia ununuzi wa vyombo vya Kwaya ya Uinjilisti ya Sayuni ,ambapo Katibu
wa kamati ya uinjilisti usharikani hapo Mzee Mboya alitoa hamasa ya kwamba ni vizuri
waliochukua kadi kuonana na viongozi wa kwaya wafanye marejesho yao kwa
minajili ya malengo yaliyowekwa yaweze kutimia.
Mzee Mboya akihamasisha washarika waliochukua kadi kutimiza ahadi zao.
Kwaya
ya Sayuni tunawashukuru wote waliorejesha michango yao na tunaomba Mungu awabariki wale ambao
awajatoa waweze kutoa kwa wakati ambapo tuliweka siku ya mwisho ya kukamilisha
ahadi ni tarehe 27/5/2018.


Comments
Post a Comment